Haingii peponi mkata udugu
Kutoka kwa Jubairi bin Mutwim -Radhi za Allah ziwe juu yake- Yakwamba yeye alimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Haingii peponi mkata udugu".
Search and read verified Prophetic hadeeth translations, explanations, benefits, categories and source attribution. Page 35.
Smart instant results tolerate minor spelling mistakes, with every filter in one place.
Kutoka kwa Jubairi bin Mutwim -Radhi za Allah ziwe juu yake- Yakwamba yeye alimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Haingii peponi mkata udugu".
Imepokewa kutoka kwa Hudhaifa -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Haingii peponi mfitinishaji".
Na imepokelewa kutoka kwa bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake -kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake - amesema: "Hamtazami Mwenyezi Mungu mwenye kuburuza nguo yake kwa kiburi".
Kutoka kwa Abuu Dardai Radhi za Allah ziwe juu yake kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake Amesema: "Hakuna kitu chenye uzito zaidi katika mizani ya muumini siku ya Kiyama kuliko tabia njema, na hakika Mwenyezi Mungu anamchukia mtu muovu mwenye kauli chafu".
Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maliki -Radhi za Allah ziwe juu yake- : Yakwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake Amesema: "Atakayependa kukunjuliwa katika riziki yake, na acheleweshewe ajali yake, basi na aunge udugu wake".
kutoka kwa Abuu Swirma -Radhi za Allah ziwe juu yake- Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayedhuru Mwenyezi Mungu naye atamdhuru, na atakayewatia watu ugumu Mwenyezi Mungu naye atamtilia ugumu".
Kutoka kwa Abdul Rahman Bin Abii Laila amesema: Alikutana nami Ka'bu bin Ujza, akasema: Hivi wataka nikupe zaidi? Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake alitoka kwetu sisi, tukasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tumekwishafahamu ni vipi tutakusalimu, sasa ni vipi t…
Kutoka kwa Ubaada bin Swaamit -Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume -Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Hana swala yeyote ambaye hakusoma sura kifunguzi cha kitabu (suratul faatiha)".
Kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa katika maradhi yake ambayo hakuweza kuamka tena: "Amewalaani Mwenyezi Mungu Mayahudi na Wakristo, waliyafanya makaburi ya Manabii wao kuwa mahali pa…
Imepokelewa kutoka kwa Abdallahi bin Masudi -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Si miongoni mwetu atakayepiga mashavu, na akachana mifuko, na akaomboleza kwa maombolezo ya watu wa zama za ujinga".
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake-yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Palipo karibu zaidi kwa mja na Mola wake ni pale anapokuwa kasujudu,Basi zidisheni dua".
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakaye koga siku ya Ijumaa josho la janaba, kisha akatoka katika saa ya kwanza ni kana kwamba katoa sadaka ya ngamia, na atakayetoka katika saa ya pili ni ka…
Follow any language without creating an account.