Atakaye koga siku ya Ijumaa josho la janaba, kisha akatoka katika saa ya kwanza ni kana kwamba katoa sadaka ya ngamia
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakaye koga siku ya Ijumaa josho la janaba, kisha akatoka katika saa ya kwanza ni kana kwamba katoa sadaka ya ngamia, na atakayetoka katika saa ya pili ni kana kwamba katoa sadaka ya ng'ombe, na atakayetoka katika saa ya tatu ni kana kwamba katoa sadaka ya kondoo, na atakayetoka katika saa ya nne ni kana kwamba katoa sadaka ya kuku, na atakaye kwenda katika saa ya tano ni kama katoa yai, akitoka imamu Malaika wanahudhuria kusikiliza ukumbusho".
Explanation
Ya kwanza: Atakayeoga josho kamili, kama kuoga janaba, kisha akaenda katika msikiti wa Ijumaa katika saa ya kwanza, ni kama katoa sadaka ya ngamia.
Ya pili: Mwenye kwenda saa ya pili ni kama katoa sadaka ya ng'ombe.
Ya tatu: Yeyote atakayekwenda saa ya tatu ni kama ametoa sadaka kondoo dume mwenye pembe.
Ya nne: Mwenye kwenda katika saa ya nne ni kama ametoa sadaka kuku.
Ya tano: Mwenye kwenda saa tano, ni kama ametoa yai katika sadaka.
Anapotoka imamu kwenda kutoa hotuba; Malaika waliokaa milangoni huacha kuwaandikia thawabu wale wanaoingia msikitini mmoja mmoja, na huja kusikiliza ukumbusho na hotuba.
Benefits
Fadhila za kuwahi swala ya Ijumaa kuanzia saa za mwanzo wa mchana.
Himizo la kwenda mbio katika matendo mema.
Malaika huhudhuria swala ya Ijumaa na kusikiliza hotuba.
Malaika wako katika milango ya misikiti, wakiwaandikia wale wanaokuja, mmoja baada ya mwingine, wanapokuja kwa ajili ya Swala ya Ijumaa.
Amesema bin Rajab: Kauli yake: “Mwenye kuoga siku ya Ijumaa kisha akaondoka” Inaashiria kuwa josho lililopendekezwa kwa siku ya Ijumaa linaanza kwa kuchomoza alfajiri, na mwisho wake ni muda wa kwenda katika swala ya Ijumaa.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

