Si miongoni mwetu atakayepiga mashavu, na akachana mifuko, na akaomboleza kwa maombolezo ya watu wa zama za ujinga
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Imepokelewa kutoka kwa Abdallahi bin Masudi -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Si miongoni mwetu atakayepiga mashavu, na akachana mifuko, na akaomboleza kwa maombolezo ya watu wa zama za ujinga".
Explanation
La kwanza: Atakayepiga mashavu, na ametaja mashavu pekee kwa sababu ndio watu hufanya mara nyingi katika hilo, na vinginevyo kupiga sehemu zingine kunaingia ndani uso.
La pili: Kuchana uwazi wa nguo ili aingize kichwa kwa sababu ya huzuni kubwa.
La tatu: Akaomboleza kwa maombolezo ya za zama za ujinga kama kujiombea maangamivu na laana, na malalamiko, na makelele na mengineyo.
Benefits
Ulazima wa kuwa na subira katika msiba, na uharamu wa kuchukizwa na kadari za Mwenyezi Mungu zenye kuumiza, na kulidhihirisha hilo: Kwa kulia kwa malalamiko au makelele au kunyoa, au kuchana nguo au mengineyo.
Uharamu wa kuwaiga watu wajinga kwa mambo yao ambayo sheria imeyathibitisha kwao.
Hakuna tatizo kuhuzunika na kulia, kwani hili halipingani na subira juu ya makadirio ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, bali ni huruma aliyoiweka Mwenyezi Mungu katika nyoyo za ndugu wa karibu na vipenzi.
Ni lazima kwa muislamu kuridhia maamuzi ya Mwenyezi Mungu, na asiporidhia basi kusubiri ni wajibu.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

