Si miongoni mwetu atakayetafuta kujua habari za mikosi au akafanyiwa, au akafanya ukuhani au akafanyiwa, au akaroga au akarogewa
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Imepokewa kutoka kwa Imran bin Huswain - Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Si miongoni mwetu atakayetafuta kujua habari za mikosi au akafanyiwa, au akafanya ukuhani au akafanyiwa, au akaroga au akarogewa, na atakayefunga fundo lolote, na atakayemuendea kuhani na akamsadikisha kwa yale ayasemayo atakuwa amekufuru yale yaliyoteremshwa kwa Muhammadi Rehema na amani ziwe juu yake".
Explanation
La kwanza: "Si miongoni mwetu atakayetafuta kujua habari za mikosi au akafanyiwa" Na asili ya hili: Ni kumuachia ndege wakati wa kuanza kazi kama safari au biashara au mengineyo, akiruka upande wa kulia anajipa matumaini na anaendelea na analolitaka, na akirukia upande wa kushoto anaamini ni mkosi anaacha alichokikusudia, haifai kufanya hivi au kumlipa mwenye kumfanyia hivi, na inaingia hapa kupiga bao kwa kitu chochote sawa sawa chenye kusikika au kuonekana, kama ndege au wanyama au wenye ulemavu au namba au siku au mengineyo.
La pili: "Atakayefanya ukuhani au akafanyiwa" Atakayedai kujua elimu ya yaliyofichikana kwa kutumia nyota na vinginevyo, au akaja kwa anayedai kujua elimu ya yaliyofichikana kama kuhani na mfano wake, akamsadikisha kwa yale ayasemayo kwa kudai kwake kujua elimu ya ghaibu, basi atakuwa kakufuru yaliyoteremshwa kwa Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake.
La tatu: "Atakayeroga au akarogewa" Naye ni yule atakayefanya uchawi yeye mwenyewe, au akampa kazi atakayemfanyia uchawi; ili amnufaishe yeyote au amdhuru, au akafunga fundo lolote kwa kufunga na nyuzi na kuzirogea kwa kusoma kinga za kishirikina zilizoharamishwa na akazipuliza.
Benefits
Kudai kujua elimu ya ghaibu ni katika shirki inayopingana na tauhidi.
Uharamu wa kuwasadikisha makuhani na kuwaendea, na vinaingia hapa kusoma viganja na kusoma yaliyoandikwa kwenye vikombe na kutazamia nyota na, hata kama ni kwa kutaka kujua.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

