Tambueni kuwa pombe imekwisha haramishwa
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Imepokewa kutoka kwa Anas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake amesema: Nilikuwa nikihudumia watu vinywaji katika nyumba ya Abuu Twalha, na pombe yao wakati huo ilikuwa ni mchanganyiko, akaamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kunadi akanadi: Tambueni kuwa pombe imekwisha haramishwa, akasema: Abuu Twalha akasema kuniambia: Toka, nenda kaimwage, nikatoka nikaimwaga, ikatiririka pombe mitaro ya Madina, baadhi ya watu wakasema: Wameuliwa baadhi ya watu na pombe ikiwa tumboni mwao, Mwenyezi Mungu akateremsha: "Hapana ubaya kwa wale walioamini na akafanya matendo mema katika vile walivyokula" [Al-Maaida: 93] Mpaka mwisho wa aya.
Explanation
"Hapana ubaya kwa wale walioamini na wakafanya matendo mema katika yale waliyokula". [Al-Maaida: 93] Mpaka mwisho wa aya. Yaani: Hawana dhambi wale walioamini katika vile walivyokula na kunywa katika pombe kabla ya kuharamishwa kwake.
Benefits
Pombe: Ni jina linalokusanya kila chenye kulewesha.
Fadhii: Ni kinywaji kinachotokana na tende mbichi na tende mbivu pasina kupikwa, na Busri: Ni matunda ya tende kabla hajaanza kuiva.
Amesema bin Hajari: Amesema Mulhib: Bila shaka pombe ilimwagwa barabarani ili kutangaza kuikataa kwake na kutangaza kuiacha kwake, na hili linakuwa na masilahi makubwa kuliko kukereka kwa kuimwaga kwake barabarani.
Kumebainishwa rehema ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake, na kwamba hawahesabu watu katika kitendo kabla ya kuteremsha hukumu.
Mwenyezi Mungu Mtukufu ameharamisha pombe; kwakuwa ndani yake kuna uharibifu ambao madhara yake yanarudi katika akili na mali, na kwa sababu yake mtu hutenda madhambi mengi; kwa kutoweka akili yake.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

