Mnayafanya, enyi watu, yale mnayoyasimamia ya kuwanwyesha mahujaji na kuuimarisha msikiti Mtukufu ni kama Imani ya aliyemuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho? [Tauba: 19] Mpaka mwisho wa Aya
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Nuuman bin Bashiri radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao amesema: Nilikuwa katika Mimbari ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, mtu mmoja akasema, si jali ni amali gani nitakayoifanya baada ya Uislamu isipokuwa nitawapa maji mahujaji, na mwingine akasema: Sijali kutofanya amali yoyote baada ya Uislamu isipokuwa nitauimarisha Msikiti mtukufu, na mwingine akasema: Kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu ni bora kuliko yote mliyosema, Omari akawakemea, na akasema: Msinyanyue sauti zenu mbele ya Mimbari ya Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake, na hali yakuwa pia ni Ijumaa, lakini nitakaposwali Ijumaa nitaingia na nitamuuliza kuhusu haya mliyotofautiana kwayo, akateremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Mnayafanya, enyi watu, yale mnayoyasimamia ya kuwanwyesha mahujaji na kuuimarisha msikiti Mtukufu ni kama Imani ya aliyemuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho? [Tauba: 19] Mpaka mwisho wa Aya.
Explanation
"Mnayafanya yale mnayoyasimamia ya kuwanwyesha mahujaji na kuuamirisha msikiti mtukufu ni kama imani ya aliyemuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na akapigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu? Haziwi sawa hali za Waumini na hali za makafiri mbele ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu hawaelekezi watu wanaozidhulumu nafsi zao kwa ukafiri kwenye mambo mema." [At-Tauba: 19].
Benefits
Kuzidiana kwa matendo hulingana na namna yalivyokuja katika sheria, na wala si kulingana na jitihada za watu.
Ubora wa Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa sharti la kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho.
Amesema Nawawi: Hapa kuna karaha ya kunyanyua sauti katika misikiti siku ya Ijumaa na siku nyinginezo, na kwamba mtu haruhusiwi kunyanyua sauti si kwa swala la kielimu wala linginelo panapokuwa na mkusanyiko wa watu kwa ajili ya swala, kwa kuwa kufanya hivyo huwashawishi wengine, na wenye kuswali na wenye kumtaja Mwenyezi Mungu.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

