Nilimuona Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alikidhi haja ndogo, kisha akatia udhu na kafuta juu ya khufu zake
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Ibrahim Nakhai kutoka kwa Hammamu bin Harithi amesema: Alikwenda haja ndogo Jariri kisha akatia udhu, na kafuta juu ya khufu zake, wakasema: Kwa nini unafanya hivi? Akasema: Ndio, Nilimuona Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alikidhi haja ndogo, kisha akatia udhu na kafuta juu ya khufu zake. Amesema A'mashi: Amesema Ibrahimu: Ilikuwa ikiwashangaza sana hadithi hii; kwa sababu kusilimu kwa Jariri kulikuwa baada ya kuteremka Suratul-Maaida.
Explanation
Benefits
Amesema Nawawi: Wamekubaliana wanaozingatiwa makubaliano yao juu ya kufaa kufuta juu ya khufu mbili, safarini na nyumbani, sawa sawa iwe kwa haja au bila haja, mpaka inafaa kwa mwanamke alioko nyumbani kwake na mgonjwa asiyeweza kutembea.
Ubora wa Jariri bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake, kiasi kwamba alikuwa na kifua kipana, akistahamili kukemewa na wanafunzi wake, hata kama wamekosea katika hilo.
Kumjibu mwenye kukataa kufuta juu ya khufu mbili na akadai kuwa kulifutwa; kwa sababu hadithi ya Jariri radhi za Allah ziwe juu yake imechelewa kuliko aya ya udhu.
Kumebainishwa kwamba ni lazima kwa mwenye kukemewa jambo na akawa akiitakidi usahihi wake asimkasirikie anayemkemea, bali ajadiliane naye kulingana na dhana yake, bali ambainishie hoja yake katika hilo kwa majibu mazuri.
Kutoa ushihidi kupitia historia wakati wa haja ya kufanya hivyo.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

