Alikuwa kituamrisha tunapokuwa safarini tusivue khofu zetu kwa siku tatu (mchana na usiku) isipokuwa kwa ajili ya janaba, lakini ni kwa haja kubwa na ndogo na usingizi
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Zirri bin Hubaishi amesema: Nilikwenda kwa Swafwan bin Assali Al-Muraadi, ili nimuulize kuhusu kufuta juu ya khofu mbili, akasema: Ni nini kimekuleta ewe Zirri? Nikasema: Kutafuta elimu, akasema: Hakika Malaika huweka mbawa zao kwa mwenye kutafuta elimu; kwa kuridhishwa na kile anachokitafuta, basi nikasema: Hakika mimi nimepata uzito ndani ya kifua changu kuhusu kufuta juu ya khofu mbili baada ya kukidhi haja ndogo na kubwa, na wewe ulikuwa miongoni mwa wanafunzi wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, hivyo nimekuja kukuuliza: Je, uliwahi kumsikia akizungumza chochote kuhusu hilo? Akasema: Ndiyo, Alikuwa kituamrisha tunapokuwa safarini tusivue khofu zetu kwa siku tatu (mchana na usiku) isipokuwa kwa ajili ya janaba, lakini ni kwa haja kubwa na ndogo na usingizi, nikasema: Je, uliwahi kumsikia akizungumza chochote kuhusu matamanio? Akasema: Ndiyo, tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika safari, wakati tukiendelea kuwa naye ghafla, Bedui mmoja alimuita kwa sauti kubwa na ya juu. Ewe Muhammadi!!!, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamjibu kwa mfano wa sauti yake: "Ehee, niambie!" Tukasema kumwambia koma!, punguza sauti yako, kwani hapa uko mbele ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na umekatazwa kufanya hivi, akasema: Wallahi siwezi kupunguza, kisha Bedui akasema: Utakuta mtu anawapenda watu fulani lakini hajawahi kukutana nao, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Mtu atakuwa pamoja na yule anayempenda siku ya Kiyama" Basi akaendelea kutusimulia mpaka akautaja mlango ulioko Magharibi mwendo wa upana wake, au anaweza kutembea aliyepanda kwenye upana wake kwa miaka arobaini au sabini.
Explanation
Benefits
Kumebainishwa pupa ya wanafunzi wa Maswahaba katika kutafuta elimu kutoka kwa Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao.
Kufaa kufuta juu ya khofu mbili, na muda wake: Kwa msafiri ni siku tatu (ikiwa ni pamoja na usiku wake), na kwa mkazi siku moja (masaa 24).
Kufuta khofu mbili kunakuwa katika hadathi ndogo pekee.
Inafaa kwa muulizaji kumuomba msomi ushahidi wa kile alichozungumza, je ni nukuu za maandiko au ni jitihada zake, na kwa msomi asijisikie vibaya kwa hilo.
Kuwa na adabu na wanachuoni na watu wema, na kushusha sauti katika vikao vya kielimu.
Kumfundisha asiyejua adabu nzuri na misingi ya tabia njema.
Himizo la kujifunza kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika upole wake, na tabia zake njema, na kuzungumza kwake na watu kulingana na uelewa wao na akili zao.
Amesema Mubaarakafuri: Hapa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alinyanyua sauti yake kama sehemu ya kumhurumia ili zisiporomoke amali zake kutokana na kauli yake Mtukufu: "Msinyanyue sauti zenu juu ya sauti ya Nabii"; akampa udhuru kwa sababu ya ujinga wake, na alinyanyua Mtume rehema na amani ziwe juu yake sauti yake mpaka ikawa mfano wa sauti yake au juu yake zaidi kwa sababu ya huruma yake iliyopita kiasi kwake.
Kuwa na pupa ya kukaa na watu wema na kuwa karibu nao na kuwapenda.
Amesema Nawawi: Na si lazima mtu kuwa nao mpaka daraja yake na malipo yake yawe mfano wao kwa namna zote.
Kufungua mlango wa matumaini na matarajio, na kutoa habari njema ya kusalimika, na kuwa mpole katika mawaidha.
Upana wa rehema ya Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, na kufungua kwake mlango wa toba.
Himizo la kufanya haraka kuomba toba na kuihesabu nafsi na kurejea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

