Nilikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake akafika katika jalala la watu fulani akakidhi haja ndogo akiwa kasimama,
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Hudhaifa -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake akafika katika jalala la watu fulani akakidhi haja ndogo akiwa kasimama, nikasimama kando naye, alipomaliza akasema: “Sogea karibu” nikasogea mpaka nikasimama karibu naye, akatawadha, kisha akapangusa juu ya soksi (Khufu) zake.
Explanation
Basi Hudhaifa akajisogeza mbali naye, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamwambia: Njoo karibu, basi Hudhaifa akamkaribia mpaka akasimama nyuma yake, nyuma ya miguu yake; Ili awe kama mstara kwake kutokana na watu kumtazama katika hali ile.
Kisha akatawadha, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, na wakati wa kuosha miguu yake, alitosheka kwa kupangusa juu ya soksi (Khofu) zake - nazo ni zile zinazovaliwa miguuni, zilizotengenezwa kwa ngozi nyembamba na mfano wake na zinazofunika vifundo vya miguu, na wala hakuzivua.
Benefits
Inafaa kukidhi haja wima, kwa sharti asidondokewe na chochote.
Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alichagua Jalala, ambapo ni mahali pa kutupia taka za wafagiaji, kwa sababu huwa ni rahisi, na haja ndogo huwa hairudi tena kwa mkojoaji.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

