Swala ya mtu katika jamaa inazidi swala yake sokoni kwake na nyumbani kwake kwa daraja zaidi ya ishirini
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Swala ya mtu katika jamaa inazidi swala yake sokoni kwake na nyumbani kwake kwa daraja zaidi ya ishirini, na hii ni pale mmoja wao atakapo tawadha…

