Safu bora kwa wanaume ni safu ya kwanza, na safu yenye shari ni ya nyuma, na safu bora kwa wanawake ni safu ya mwisho na yenye shari ni safu ya mwanzo
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Safu bora kwa wanaume ni safu ya kwanza, na safu yenye shari ni ya nyuma, na safu bora kwa wanawake ni safu ya mwisho na yenye shari ni safu ya mwanzo"
Explanation
Benefits
Inafaa wanawake kuswali msikitini pamoja na wanaume katika safu zao binafsi, lakini kwa kujistiri na kujiheshimu.
Wanawake wakikusanyika msikitini, basi wanatakiwa wapange safu, kama safu za wanaume, na wala wasitengane, bali wanatakiwa kushikana katika safu na kuziba nyufa, kama ilivyo katika safu za wanaume.
Kumebainishwa namna sheria ilivyotilia umuhimu kwa kuhimiza kujiweka mbali wanawake na wanaume mpaka katika mahali pa ibada.
Kutofautiana kwa watu ni kwa sababu ya matendo yao.
Amesema Nawawi: Ama safu za wanaume kwa ujumla wake bora zaidi kuliko zote ni ile ya kwanza, na mbaya zaidi ni safu za mwisho, na ama safu za wanawake kilichokusudiwa katika hadithi ni: Safu za wanawake wanaoswali pamoja na wanaume, lakini wakiswali kwa peke yao na si pamoja na wanaume, basi hapo ni kama wanaume; safu yao bora zaidi ni safu ya kwanza na ya shari zaidi ni ya mwisho.
Amesema Nawawi: Safu ya kwanza iliyosifiwa zikaja fadhila zake katika hadithi na kuihimiza ni safu inayofuata nyuma ya imam; sawa sawa mtu aje mapema au kwa kuchelewa, na sawa iwe kamili au pungufu na mfano wake au la.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

