Imekuwa ni bora swala ya wengi kuliko swala ya mmoja wenu peke yake, kwa vipengele ishirini na tano, na hukusanyika Malaika wa usiku na Malaika wa mchana katika swala ya Alfajiri
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Imekuwa ni bora swala ya wengi kuliko swala ya mmoja wenu peke yake, kwa vipengele ishirini na tano, na hukusanyika Malaika wa usiku na Malaika wa mchana katika swala ya Alfajiri" Kisha anasema Abuu Huraira: Someni mkitaka: "Hakika Qur'ani ya Alfajiri hushuhudiwa" [Al-Israa: 78].
Explanation
Someni mkitaka: "Hakika Qur'ani ya Alfajiri hushuhudiwa" [Al-Israa: 78] Yaani: Qur'ani ya Alfajiri huishuhudia Malaika wa usiku na Malaika wa mchana.
Benefits
Hapa kuna fadhila ya swala ya Alfajiri; kwa kufanywa pekee kukusanyika kwa Malaika ndani yake.
Amesema bin Bazi: Ni wajibu kwa muumini awe na pupa ya kuhifadhi swala katika jamaa hata kama nyumba yake itakuwa mbali, ili aipate kheri hii kubwa.
Amesema Nawawi katika kukusanya kati ya riwaya ya kwamba swala ya jamaa ni bora kuliko swala ya mtu mmoja kwa daraja ishirini na tano, na nyingine kwa daraja ishirini na saba: Na kukusanya kati ya kauli hizi mbili ni kwa sura tatu: Ya kwanza: Hazipingani, kwani kutajwa kidogo hakupingani na wingi, na maana ya idadi haizingatiwi kwa wasomi wa misingi ya sheria. Ya pili: Yawezekana alieleza kidogo kisha Allah Mtukufu akamjulisha ziada ya fadhila, naye akaieleza. Ya tatu: Nikuwa zinatofautiana kulingana na kutofautiana kwa wenye kuswali, baadhi yao wanakuwa na ishirini na tano, na baadhi yao ishirini na saba kulingana na ukamilifu wa swala na kuihifadhi kwake na muonekano wake na utulivu wake na wingi wa mkusanyiko wake na ubora wao na utukufu wa eneo na mfano wa hayo, na Allah ndiye mjuzi zaidi.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

