Hakika Peponi kuna Soko, watakuwa wakienda hapo kila siku ya Ijumaa
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maliki radhi za Allah ziwe juu yake: Ya kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Hakika Peponi kuna Soko, watakuwa wakienda hapo kila siku ya Ijumaa, basi utavuma upepo wa kaskazi utawamwagikia katika nyuso zao na nguo zao, na hapo wataongezeka uzuri na urembo, watarudi kwa familia zao wakiwa wameongezeka uzuri na urembo, watasema kuwaambia: Wallahi mmezidi uzuri na urembo baada yetu, watasema: Na nyinyi Wallahi hakika mmezidi uzuri na urembo baada yetu".
Explanation
Benefits
Hadithi hizi zinampelekea mtu kuwa na hamu ya kutenda mema ambayo hutumika kumfikisha mtu katika nyumba hii.
Ameutaja upepo wa kaskazi pekee; kwa sababu ndio uliokuwa upepo mzuri zaidi kwa waarabu kwani ndio ulikuwa ukija na kheri na mvua.
Himizo la kuwaita watu kwa Mwenyezi Mungu kwa kuwahamasisha kuhusu pepo na neema zake.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

