Hili ni jiwe lililotupwa Motoni muda wa (miaka) sabini iliyopita, na sasa linaanguka Motoni mpaka litafika katika kina chake
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake ghafla akasikia kishindo, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: “Je, mnajua ni nini hiki?” Akasema: Tukasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanajua zaidi, akasema: «Hili ni jiwe lililotupwa Motoni muda wa (miaka) sabini iliyopita, na sasa linaanguka Motoni mpaka litafika katika kina chake.
Explanation
Akawaambia rehema na amani ziwe juu yake: Sauti hii mliyoisikia ni ya jiwe lililorushwa kutoka ukingo wa Jahannam miaka sabini iliyopita lilikuwa likiporomoka na kuanguka humo, hivi sasa mliposikia kishindo ndio limefika katika kina chake.
Benefits
Ni sunna kuiegemeza elimu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika yale ambayo mtu hana elimu nayo.
Mwalimu anatakiwa kuamsha hisia na umakini kwa wanafunzi kabla ya kuwaeleza; ili uwe ni msukumo wa wao kuelewa.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

