Hakika mmoja wenu hukusanywa umbile lake ndani ya tumbo la mama yake siku arobaini
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Imepokewa kutoka kwa Abuu Abdirahman Abdullahi Bin Masoud radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alituhadithia Mtume rehema na amani ziwe juu yake naye ndiye mkweli mwenye kusadikika: "Hakika mmoja wenu hukusanywa umbile lake ndani ya tumbo la mama yake siku arobaini, kisha linakuwa pande la damu kwa mfano wake, kisha linakuwa pande la nyama mfano wake (siku arobaini), kisha linatumiwa Malaika analipulizia roho, na anaamrishwa kuandika maneno manne: Kuandika riziki yake, na umri wake, na matendo yake, na kuwa ni muovu au mwema; namuapa yule ambaye hakuna Mola isipokuwa yeye hakika mmoja wenu atafanya amali za watu wa Peponi mpaka ikawa baina yake na Peponi ni dhiraa moja (futi) kikamtangulia kitabu akafanya amali za watu wa motoni akauingia, na hakika mmoja wenu atafanya amali za watu wa motoni mpaka ikawa baina yake na Moto isipokuwa dhiraa, kitabu kikamtangulia akafanya amali za watu wa Peponi na akaingia".
Explanation
Benefits
Kuamini hukumu na kadari.
Mwisho wa mambo yote huwa kwa namna ambavyo imekwishapangwa na kukadiriwa.
Tahadhari ya kutodanganyika na muonekano wa matendo; Bali matendo huangaliwa mwisho wake.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

