Majaribio hayaachi kumpata muumini wa kiume na muumini wa kike katika nafsi yake, na watoto wake, na mali yake mpaka atakapokutana na Mwenyezi Mungu ilhali hana dhambi hata moja
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Majaribio hayaachi kumpata muumini wa kiume na muumini wa kike katika nafsi yake, na watoto wake, na mali yake mpaka atakapokutana na Mwenyezi Mungu ilhali hana dhambi hata moja."
Explanation
Benefits
Balaa pekee linafuta madhambi ila kwa sharti la imani, hivyo akisubiri mja na akawa hakulalamika basi analipwa.
Himizo la subira katika mambo yote, katika yale ayapendayo na anayoyachukia, awe na subira mpaka atekeleze aliyoyaamrisha Mwenyezi Mungu, na awe na subira mpaka akae mbali na yale aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu, akitaraji malipo ya Mwenyezi Mungu na kuogopa adhabu yake.
Kauli yake: “Kwa muumini mwanaume na mwanamke,” kuongeza neno “muumini wa kike” ndani yake ni ushahidi wa kutiliwa mkazo zaidi kwa wanawake. Vinginevyo, lau angesema: "Kwa muumini wa kiume," mwanamke angejumuishwa ndani yake; Kwa sababu hii si mahsusi kwa wanaume, basi ikiwa dhiki itampata mwanamke, naye anaahidiwa malipo kama hayo kwa kufutiwa madhambi na makosa.
Hili ni miongoni mwa mambo yanayomtia faraja mtu kwa yale anayokumbana nayo katika maumivu kila mara yanayosababishwa na mabalaa.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

