Ukipenda unaweza kuvumulia na utapata malipo ya Pepo, na ukitaka nitakuombea kwa Mwenyezi Mungu akuponye
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa bin Abbasi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, yeye na baba yake: Ya kwamba pindi aliposema kumwambia Atwaa bin Abii Rabaahi: Hivi je, nikuonyeshe mwanamke miongoni mwa wanawake wa Peponi? Nikasema: Ndio, akasema: Huyu mwanamke mweusi, alikuja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Hakika mimi huanguka, na nguo zangu hufunuka ninapoanguka, nakuomba uniombee kwa Mwenyezi Mungu, akasema: "Ukipenda unaweza kuvumulia na utapata malipo ya Pepo, na ukitaka nitakuombea kwa Mwenyezi Mungu akuponye" Akasema: Bali nitavumilia, akasema: Lakini mimi huwa nafunuka nguo, basi niombee kwa Mwenyezi Mungu nisifunuke, basi akamuombea.
Explanation
Benefits
Amesema Nawawi: Na hapa kuna ushahidi kuwa ugonjwa wa kuanguka kwa mtu hulipwa malipo yaliyokamilika
Tazama heshima na haya kwa wanawake wa kiswahaba, na pupa yao juu ya kujisitiri, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, mwanamke huyu, kubwa zaidi alilokuwa akilihofia ni kufunuka sehemu ya mwili wake.
Amesema bin Hajari: Kuchukua jambo gumu ni bora kuliko kuchukua ruhusa, kwa mtu atakayejua kuwa anauwezo wa kulibeba, na hatodhoofika kwa kulibeba gumu hilo.
Amesema bin Hajari: Na hapa nikuwa; tiba ya maradhi yote ni kwa dua na kuelekea kwa Mwenyezi Mungu, hufaa zaidi na kunufaisha zaidi kuliko tiba ya miti shamba (madawa), na kwamba athari ya hilo na muitikio wa mwili ni mkubwa zaidi kuliko athari ya dawa za mwili, lakini huleta ahueni kwa mambo mawili: La kwanza: Upande wa mgonjwa, kuwa na imani ya kweli na Mwenyezi Mungu, na la pili: Upande wa tabibu, kuwa na nguvu kubwa ya kuelekea kwa Mwenyezi Mungu, na kuwa na nguvu kubwa ya uchamungu, na kumtegemea Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu Ndiye Mjuzi zaidi.
Amesema bin Hajari: Hapa kuna ushahidi juu ya kuacha kutumia dawa.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

