Mwenyezi Mungu alipoumba Pepo na Moto alimtuma Malaika Jibril -Amani iwe juu yake- aende peponi
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Abuu Huraira -Allah amridhie- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Mwenyezi Mungu alipoumba Pepo na Moto alimtuma Malaika Jibril -Amani iwe juu yake- aende peponi Akamwambia: Iangalie hiyo pepo na yale niliyo waandalia humo watu wa peponi, basi Jibrili akaiangalia Pepo kisha akarudi, akasema: Naapa kwa utukufu Wako ewe Mwenyezi Mungu hatozisikia mtu yeyote habari za pepo kisha asiingie humo, kisha akamuamrisha kuizungushia Pepo hiyo mambo yenye kuchukiza, kisha akamwambia nenda tena ukaiangalie na uangalie yale niyowaandalia
watu wake humo peponi. Basi akaiangalia ghafla akaiona imezungushwa vyenye kuchukiza, akasema: Naapa kwa utukufu Wako kwa hakika ninahofia kuwa hatoingia mtu yeyote. Akasema kumwambia Jibrili nenda na uuangalie Moto na yale niliyo waandalia humo watu wa Motoni. Basi akauangalia Moto na akauona Moto ulivyopambwa, basi akarudi na akasema: Naapa kwa utukufu Wako hatoingia yeyote humo, basi akaamrisha ukazungushwa mambo yenye kutamanisha, basi akamwambia: Rudi na uuangalie tena. Basi akauangalia akaukuta umepambwa na kuzungushwa yenye kutamanisha, basi akarudi na akasema: Naapa kwa utukufu wako kwa hakika nahofia yakuwa hatosalimika mtu yeyote isipokuwa ataingia Motoni."
Explanation
Benefits
Ulazima wa kuamini mambo ya ghaibu (yasiyo onekana), na kuamini kila kilichokuja kutoka kwa, Mwenyezi Mungu na Mtume wake -Rehema na amani ziwe juu yake-.
Umuhimu wa kusubiri kwenye mambo yenye kuudhi kwa sababu hiyo ni njia ya kumfikisha mtu peponi.
Umuhimu wa kujiepusha na mambo yaliyoharamishwa; kwa sababu hiyo ni njia ya kumfikisha mtu Motoni.
Pepo imezungushwa yenye kuchukiza, na Moto umezungushwa yenye kutamanisha, nayo hupelekea kuingia kwenye majaribu katika maisha haya ya Duniani.
Njia ya kwenda Peponi ni ngumu na ina tabu nyingi, na inahitajia subira kuvumilia mateso pamoja na kuwa na imani, na njia ya kwenda Motoni imejaa vyenye kuvutia na kutamanisha hapa duniani.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

