Hakika kundi la kwanza la watu watakaoingia peponi watakuwa katika sura ya mwezi usiku wa tarehe kumi na tano, kisha wale wanaowafuata watakuwa katika sura ya nyota kali ing'aayo na iangazayo mbinguni
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika kundi la kwanza la watu watakaoingia peponi watakuwa katika sura ya mwezi usiku wa tarehe kumi na tano, kisha wale wanaowafuata watakuwa katika sura ya nyota kali ing'aayo na iangazayo mbinguni, hawatokwenda haja ndogo wala kubwa, na wala hawatotema mate wala kupenga kamasi, vitana vyao vitakuwa vya dhahabu, jasho lao litakuwa ni miski, na vitezo vyao vitakuwa vikinukia udi wenye harufu nzuri mno, udi wa marashi, na wake zao watakuwa ni katika Mahurulaini, na wote watakuwa katika umbile la mtu mmoja, watakuwa katika sura ya baba yao Adam, urefu kwenda juu ni dhiraa sitini (Dhiraa moja ni inchi 18)".
Explanation
Benefits
Kutumia mfumo wa kufananisha katika kusogeza karibu maana na kuifafanua.
Amesema Qurtubi: Huenda mtu anaweza kusema kuna haja gani ya wao kuwa na machanuo hali yakuwa wameumbwa upya na nywele zao hazichafuki? Na wana haja gani ya wao kuwa na udi na hali yakuwa harufu yao ni nzuri kuliko miski? Akasema: Na linajibiwa hilo kuwa: Neema za watu wa peponi kama kula na kunywa na kuvaa na marashi hivi vyote havitakuwa kwa sababu ya maumivu ya njaa au kiu au uchi au harufu mbaya, bali ni ladha mfululuzo na neema mfululuzo, na hekima katika hilo nikuwa wao wataneemeka kwa aina mbali mbali ambazo walikuwa wakineemeka nazo katika dunia.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

