Nilionyeshwa Pepo na Moto, katu sijawahi kuona katika kheri na shari mfano wa siku hiyo, na lau mngejua ninayoyajua basi mngelicheka kidogo na mngelia sana
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Anasi bin Maliki radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Lilimfikia jambo Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka kwa Maswahaba zake, akawahutubia akasema: "Nilionyeshwa Pepo na Moto, katu sijawahi kuona katika kheri na shari mfano wa siku hiyo, na lau mngejua ninayoyajua basi mngelicheka kidogo na mngelia sana" Akasema: Haikuwahi kutokea kwa Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake siku ngumu kama hiyo, akasema: Wakafunika nyuso zao huku wakitoa sauti za kugugumia (kwa vilio), anasema: Akasimama Omari akasema: Tumemridhia Mwenyezi Mungu kuwa Mola, na Uislamu kuwa dini, na Muhammadi kuwa Nabii, anasema: akasimama yule bwana akasema: Ni nani baba yangu? Akasema: "Baba yako ni fulani", ikateremka: "Enyi mlioamini! Msiulize mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni" [Al-Maaida: 101].
Explanation
Akasema: "Baba yako ni fulani", ikateremka: "Enyi mlioamini! Msiulize kuhusu mambo ambayo yakikudhihirikieni yatakuchukizeni" [Al-Ma’idah: 101].
Benefits
Waliathirika na mawaidha Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao, na hofu yao kubwa dhidi ya adhabu za Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka.
Sunna ya kufunika uso wakati wa kulia.
Amesema Al-Khattwabi: Hadithi hii ni kwa mtu aliyeuliza kwa kuchokonoa mambo au kwa ukaidi katika mambo ambayo hana haja nayo, ama atakayeuliza kwa dharura, kwa kutokewa na jambo akaliulizia, huyu hana dhambi juu yake wala lawama.
Himizo la kuwa na msimamo katika kumtii Allah, na kujitenga mbali na kumuasi Allah, na kusimama katika mipaka ya Mwenyezi Mungu.
Hapa inaonyesha kufaa kukasirika wakati wa mawaidha na wakati wa kufundisha.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

