Atakayetoa vitu vya namna mbili katika njia ya Mwenyezi Mungu huitwa katika milango ya pepo, ewe mja wa Mwenyezi Mungu hii ni kheri, atakayekuwa miongoni mwa watu wa swala ataitwa katika mlango wa swala, atakayekuwa katika watu wa jihadi ataitwa katika mlango wa jihadi
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- hadithi Marfu'u: "Atakayetoa jinsia (aina) mbili katika njia ya Mwenyezi Mungu huitwa katika milango ya pepo, ewe mja wa Mwenyezi Mungu hii ni kheri, hivyo atakayekuwa miongoni mwa watu wa swala ataitwa katika mlango wa swala, atakayekuwa katika watu wa jihadi ataitwa katika mlango wa jihadi, atakayekuwa miongoni mwa watu wa swaumu ataitwa katika mlango wa Rayyan, atakayekuwa miongoni mwa watu wa sadaka ataitwa katika mlango wa sadaka" Akasema Abuubakari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Namuweka fidia baba yangu na mama yangu kwaajili yako, ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! je kama kuna mtu ataitwa katika milango hiyo akawa na dharura, je anaweza kuitwa mtu katika milango hiyo yote? basi akasema: "Ndiyo, na ninataraji wewe utakuwa miongoni mwao".
Explanation
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

