Atakapokunywa mbwa katika chombo cha mmoja wenu basi akioshe mara saba
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakapokunywa mbwa katika chombo cha mmoja wenu basi akioshe mara saba". Na kwa Muslim: "Moja kati ya mara hizo aoshe kwa udogo"
Explanation
Benefits
Mbwa kulamba katika chombo, kunakitia najisi chombo hicho, na kunanajisisha maji yaliyoko ndani yake.
Kusafisha kwa udongo na kurudia mara saba hii ni maalum kwa kusafisha pale atakapo lamba, lakini si katika mkojo wake na uchafu wake na vyote atakavyovichafua mbwa.
Jinsi ya kuosha chombo kwa udongo: Ataweka maji ndani ya chombo na kuongeza udongo ndani yake, kisha atasafisha chombo kwa mchanganyiko huu.
Maana ya dhahiri ya Hadith ni kuwa hadithi hii inajumuisha mbwa wote, hata mbwa ambao sheria imeruhusu kufugwa, kama vile kuwinda, kulinda, na mbwa wa mifugo.
Sabuni na majani ya miti havichukui nafasi ya udongo; Kwa sababu Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliweka sharti la kutumia udongo.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

