Sub-haana llaah, ametakasika Mwenyezi Mungu, hakika muumini hanajisiki
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Ya kwamba alikutana na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika barabara miongoni mwa barabara za mji wa Madina huku akiwa na janaba, akamkwepa na akaenda kuoga, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamtafuta hakumpata, alipomjia akasema: "Ulikuwa wapi ewe Abuu Huraira?" Akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ulikutana nami, nami nikiwa na janaba, sikufurahishwa kukaa na wewe mpaka nioge, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Sub-haana llaah, ametakasika Mwenyezi Mungu, hakika muumini hanajisiki".
Explanation
Benefits
Usafi wa muumini akiwa hai au maiti.
Kuwaheshimu watu wenye heshima, na elimu, na utengefu, na kukaa nao kwa muonekano mzuri.
Hapa kuna sheria ya mfuasi kumuomba idhini ya kuondoka anayemfuata, kwani Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimkemea Abuu Huraira radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kwa kuondoka kwake pasina yeye kujua, na hii ni kwa sababu kuomba ruhusa ni katika adabu nzuri.
Kusema: Sub-haana llaah, ametakasika Mwenyezi Mungu, wakati wa kustaajabu.
Kufaa mtu kusimulia mambo yake binafsi katika yale ya aibu, kwa ajili ya masilahi.
Kafiri ni najisi, lakini najisi yake si ya kuonekana, kwa sababu ya uchafu wa itikadi yake.
Amesema Nawawi: Na katika hadithi hii pia kuna adabu, ya kwamba msomi atakapoona kwa anayemfuata jambo analohofia kwake kwenda kinyume na usahihi basi amuulize, na amwambie lililo sahihi, na ambainishie hukumu yake, na Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi zaidi.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

