الفجر
Al-Fajr
The Dawn
1 - Al-Fajr (The Dawn) - 001
وَٱلۡفَجۡرِ
Naapa kwa alfajiri!
Naapa kwa mwangaza wa asubuhi unapo ufukuza usiku.
2 - Al-Fajr (The Dawn) - 002
وَلَيَالٍ عَشۡرٖ
Na kwa masiku kumi!
Na kwa masiku kumi yaliyo tukuzwa na Mwenyezi Mungu. (Na hayo ni masiku kumi ya mwanzo wa Mwezi wa Alhaj, Mfungo Tatu).
3 - Al-Fajr (The Dawn) - 003
وَٱلشَّفۡعِ وَٱلۡوَتۡرِ
Na kwa viwili viwili na kimoja kimoja!
Na shafi' yaani hisabu inayo gawika kwa mbili, kama 4, 6, 8 n.k. na witri, yaani isiyo gawika kwa mbili, kama 1, 3, 5 n.k. katika kila kitu.
4 - Al-Fajr (The Dawn) - 004
وَٱلَّيۡلِ إِذَا يَسۡرِ
Na kwa usiku unapo pita!
Na kwa usiku unapo pita kwa kwenda ulimwengu kwa namna ya ajabu.
5 - Al-Fajr (The Dawn) - 005
هَلۡ فِي ذَٰلِكَ قَسَمٞ لِّذِي حِجۡرٍ
Je! Hapana katika haya kiapo kwa mwenye akili?
Je! Katika vitu vilivyo tajwa vinavyo onekana kwa akili hapana kiapo cha kukinaisha?
6 - Al-Fajr (The Dawn) - 006
أَلَمۡ تَرَ كَيۡفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِعَادٍ
Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo wafanya kina A'di?
Kwani hujui jinsi Mola wako Mlezi alivyo wateremshia adhabu yake kaumu ya Hud, ?
7 - Al-Fajr (The Dawn) - 007
إِرَمَ ذَاتِ ٱلۡعِمَادِ
Wa Iram, wenye majumba marefu?
Watu wa Iram wenye majengo marefu?
8 - Al-Fajr (The Dawn) - 008
ٱلَّتِي لَمۡ يُخۡلَقۡ مِثۡلُهَا فِي ٱلۡبِلَٰدِ
Ambao haukuumbwa mfano wake katika nchi?
Ambayo haikupata kujengwa mfano wake kwa umadhubuti na ujenzi katika nchi.
9 - Al-Fajr (The Dawn) - 009
وَثَمُودَ ٱلَّذِينَ جَابُواْ ٱلصَّخۡرَ بِٱلۡوَادِ
Na Thamudi walio chonga majabali huko bondeni?
Kwani hukujua jinsi Mola wako Mlezi alivyo teremsha adhabu yake kwa Thamudi, kaumu ya Saleh, walio chonga majabali kujengea nyumba zao huko bondeni?
10 - Al-Fajr (The Dawn) - 010
وَفِرۡعَوۡنَ ذِي ٱلۡأَوۡتَادِ
Na Firauni mwenye vigingi?
Au kwani hukujua vipi Mola wako Mlezi alivyo wateremshia adhabu yake Firauni mwenye majeshi yaliyo upa nguvu ufalme wake kama vigingi vinavyo simamisha makhema?
11 - Al-Fajr (The Dawn) - 011
ٱلَّذِينَ طَغَوۡاْ فِي ٱلۡبِلَٰدِ
Ambao walifanya jeuri katika nchi?
Ambao walipita mipaka katika nchi?
12 - Al-Fajr (The Dawn) - 012
فَأَكۡثَرُواْ فِيهَا ٱلۡفَسَادَ
Wakakithirisha humo ufisadi?
Na wakazidisha kufanya uharibifu kwa ukafiri na udhalimu?
13 - Al-Fajr (The Dawn) - 013
فَصَبَّ عَلَيۡهِمۡ رَبُّكَ سَوۡطَ عَذَابٍ
Basi Mola wako Mlezi aliwapiga mjeledi wa adhabu.
Basi Mola wako Mlezi aliwateremshia adhabu kali ya kuwaunguza.
14 - Al-Fajr (The Dawn) - 014
إِنَّ رَبَّكَ لَبِٱلۡمِرۡصَادِ
Hakika Mola wako Mlezi yupo kwenye mavizio anawavizia.
Hakika Mola wako Mlezi anaviangalia vitendo vya watu, na anawahisabia, na atakuja kuwalipa kwavyo.
15 - Al-Fajr (The Dawn) - 015
فَأَمَّا ٱلۡإِنسَٰنُ إِذَا مَا ٱبۡتَلَىٰهُ رَبُّهُۥ فَأَكۡرَمَهُۥ وَنَعَّمَهُۥ فَيَقُولُ رَبِّيٓ أَكۡرَمَنِ
Ama mtu anapo jaribiwa na Mola wake Mlezi, akamkirimu na akamneemesha, husema: Mola wangu Mlezi amenikirimu!
Ama mtu akijaribiwa na Mola wake Mlezi na akamkirimu, na akamneemesha kwa mali na cheo na nguvu, basi husema kwa kughurika na hayo: Mola wangu Mlezi amenitukuza kwa kuwa ninastahiki haya!
16 - Al-Fajr (The Dawn) - 016
وَأَمَّآ إِذَا مَا ٱبۡتَلَىٰهُ فَقَدَرَ عَلَيۡهِ رِزۡقَهُۥ فَيَقُولُ رَبِّيٓ أَهَٰنَنِ
Na ama anapo mjaribu akampunguzia riziki yake, husema: Mola wangu Mlezi amenitia unyonge!
Na pindi Mola wake Mlezi akimjaribu mtu kwa kumdhikisha riziki, basi hughafilika na hikima ya hayo na husema: Mola wangu Mlezi kanidhalilisha!
17 - Al-Fajr (The Dawn) - 017
كَلَّاۖ بَل لَّا تُكۡرِمُونَ ٱلۡيَتِيمَ
Sivyo hivyo! Bali nyinyi hamuwakirimu mayatima,
Wacheni mtindo huo! Mambo siyo hayo kama msemavyo; bali nyinyi hamumkirimu yatima;
18 - Al-Fajr (The Dawn) - 018
وَلَا تَحَـٰٓضُّونَ عَلَىٰ طَعَامِ ٱلۡمِسۡكِينِ
Wala hamhimizani kulisha masikini;
Wala hamhimizani kuwalisha masikini;
19 - Al-Fajr (The Dawn) - 019
وَتَأۡكُلُونَ ٱلتُّرَاثَ أَكۡلٗا لَّمّٗا
Na mnakula urithi kwa ulaji wa pupa,
Na mnakula mali ya urithi kwa pupa, hamchagui linalo faa na lisilo faa.
20 - Al-Fajr (The Dawn) - 020
وَتُحِبُّونَ ٱلۡمَالَ حُبّٗا جَمّٗا
Na mnapenda mali pendo la kupita kiasi.
Na mnayapenda mali mno, yanayo kupelekeeni kupapatika katika kuyakusanya na ubakhili wa kuyatumia.
21 - Al-Fajr (The Dawn) - 021
كَلَّآۖ إِذَا دُكَّتِ ٱلۡأَرۡضُ دَكّٗا دَكّٗا
Sivyo hivyo! Itakapo vunjwa ardhi vipande vipande,
Wacheni vitendo hivyo! Kwani inakungojeeni siku itapo lazwa ardhi iwe sawa sawa,
22 - Al-Fajr (The Dawn) - 022
وَجَآءَ رَبُّكَ وَٱلۡمَلَكُ صَفّٗا صَفّٗا
Na akaja Mola wako Mlezi na Malaika safu safu,
Na aje Mola wako Mlezi kama anavyo stahiki kuja kwake Subhanahu na Malaika waje kwa safu safu;
23 - Al-Fajr (The Dawn) - 023
وَجِاْيٓءَ يَوۡمَئِذِۭ بِجَهَنَّمَۚ يَوۡمَئِذٖ يَتَذَكَّرُ ٱلۡإِنسَٰنُ وَأَنَّىٰ لَهُ ٱلذِّكۡرَىٰ
Na ikaletwa Jahannamu siku hiyo, siku hiyo mtu atakumbuka! Lakini kukumbuka huko kutamfaa nini?
Na siku hiyo iletwe Jahannamu, nyumba ya adhabu, siku hiyo yatapo tokea hayo mwanaadamu atakumbuka aliyo yaharibu - lakini wapi! Kukumbuka huko kumfae nini, na wakati umekwisha pita?
24 - Al-Fajr (The Dawn) - 024
يَقُولُ يَٰلَيۡتَنِي قَدَّمۡتُ لِحَيَاتِي
Atasema: Laiti ningeli jitangulizia kwa uhai wangu!
Atasema kwa majuto: Laiti ningeli jitangulizia katika dunia vitendo vyema vya kunifaa katika maisha ya Akhera!
25 - Al-Fajr (The Dawn) - 025
فَيَوۡمَئِذٖ لَّا يُعَذِّبُ عَذَابَهُۥٓ أَحَدٞ
Basi siku hiyo hataadhibu yeyote namna ya kuadhibu kwake.
Siku hiyo zitakuwa hali hizi, haadhibu mtu kama adhabu ya Mwenyezi Mungu, wala hafungi mtu kama afungavyo Yeye.
26 - Al-Fajr (The Dawn) - 026
وَلَا يُوثِقُ وَثَاقَهُۥٓ أَحَدٞ
Wala hatafunga yeyote kama kufunga kwake.
Siku hiyo zitakuwa hali hizi, haadhibu mtu kama adhabu ya Mwenyezi Mungu, wala hafungi mtu kama afungavyo Yeye.
27 - Al-Fajr (The Dawn) - 027
يَـٰٓأَيَّتُهَا ٱلنَّفۡسُ ٱلۡمُطۡمَئِنَّةُ
Ewe nafsi iliyo tua!
Ewe nafsi uliye tulia juu ya Haki!
28 - Al-Fajr (The Dawn) - 028
ٱرۡجِعِيٓ إِلَىٰ رَبِّكِ رَاضِيَةٗ مَّرۡضِيَّةٗ
Rejea kwa Mola wako Mlezi umeridhika, na umemridhisha.
Rejea kwenye radhi ya Mola wako Mlezi nawe uradhi kwa neema ulio pewa, nawe umemridhisha kwa a'mali uliyo ikadimisha.
29 - Al-Fajr (The Dawn) - 029
فَٱدۡخُلِي فِي عِبَٰدِي
Basi ingia miongoni mwa waja wangu,
Basi ingia katika kundi la waja wangu walio wema!
30 - Al-Fajr (The Dawn) - 030