الفلق
Al-Falaq
The Daybreak
1 - Al-Falaq (The Daybreak) - 001
قُلۡ أَعُوذُ بِرَبِّ ٱلۡفَلَقِ
Sema: Najikinga kwa Mola Mlezi wa mapambazuko,
Sema najikinga na Mola Mlezi wa asubuhi inapo pambazuka kutokana na usiku.
2 - Al-Falaq (The Daybreak) - 002
مِن شَرِّ مَا خَلَقَ
Na shari ya alivyo viumba,
Na shari ya kila chenye shari katika viumbe, ambavyo hapana wa kuzuia shari yao ila Mwenye kumiliki amri yao.
3 - Al-Falaq (The Daybreak) - 003
وَمِن شَرِّ غَاسِقٍ إِذَا وَقَبَ
Na shari ya giza la usiku liingiapo,
Na shari ya usiku unapo kuwa totoro.
4 - Al-Falaq (The Daybreak) - 004
وَمِن شَرِّ ٱلنَّفَّـٰثَٰتِ فِي ٱلۡعُقَدِ
Na shari ya wanao pulizia mafundoni,
Na shari ya anaye pita baina ya watu kwa sababu ya kuwafisidi.
5 - Al-Falaq (The Daybreak) - 005