المسد

 

Al-Masad

 

The Palm Fiber

1 - Al-Masad (The Palm Fiber) - 001

تَبَّتۡ يَدَآ أَبِي لَهَبٖ وَتَبَّ
Imeangamia mikono ya Abu Lahab, na yeye pia ameangamia.
Imeteketea mikono ya Abu Lahab iliyo kuwa ikiwaudhi Waislamu, na yeye mwenyewe amehiliki pia.

2 - Al-Masad (The Palm Fiber) - 002

مَآ أَغۡنَىٰ عَنۡهُ مَالُهُۥ وَمَا كَسَبَ
Hayatamfaa mali yake, wala alivyo vichuma.
Hayatolindwa na adhabu ya Mwenyezi Mungu mali yake aliyo kuwa nayo, wala cheo chake alicho kichuma.

3 - Al-Masad (The Palm Fiber) - 003

سَيَصۡلَىٰ نَارٗا ذَاتَ لَهَبٖ
Atauingia Moto wenye mwako.
Ataingia katika Moto unao waka, aungue.

4 - Al-Masad (The Palm Fiber) - 004

وَٱمۡرَأَتُهُۥ حَمَّالَةَ ٱلۡحَطَبِ
Na mkewe, mchukuzi wa kuni,
Na ataingia pia kwenye Moto mkewe huyo aliye kuwa akibeba masengenyo baina ya watu, kama alivyo ingia yeye (mumewe).

5 - Al-Masad (The Palm Fiber) - 005

فِي جِيدِهَا حَبۡلٞ مِّن مَّسَدِۭ
Shingoni mwake iko kamba iliyo sokotwa.
Juu ya shingo yake itakuwa kamba ya mtende ya kumtesa.

[sc name="verse"][/sc]

Scroll to Top