الكافرون
Al-Kafirun
The Disbelievers
1 - Al-Kafirun (The Disbelievers) - 001
قُلۡ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلۡكَٰفِرُونَ
Sema: Enyi makafiri!
Ewe Muhammad! Sema: Enyi makafiri, mlio shikilia juu ya ukafiri wenu.
2 - Al-Kafirun (The Disbelievers) - 002
لَآ أَعۡبُدُ مَا تَعۡبُدُونَ
Siabudu mnacho kiabudu;
Mimi simuabudu mnaye muabudu nyinyi badala ya Mwenyezi Mungu.
3 - Al-Kafirun (The Disbelievers) - 003
وَلَآ أَنتُمۡ عَٰبِدُونَ مَآ أَعۡبُدُ
Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu.
Wala nyinyi si wenye kumuabudu huyo ambaye mimi namuabudu, naye ni Mwenyezi Mungu wa pekee.
4 - Al-Kafirun (The Disbelievers) - 004
وَلَآ أَنَا۠ عَابِدٞ مَّا عَبَدتُّمۡ
Wala sitaabudu mnacho abudu.
Wala mimi si mwenye kuabudu mfano wa ibada yenu, kwani nyinyi ni washirikina.
5 - Al-Kafirun (The Disbelievers) - 005
وَلَآ أَنتُمۡ عَٰبِدُونَ مَآ أَعۡبُدُ
Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu.
Wala nyinyi si wenye kuabudu mfano wa ibada yangu, kwani hii ni Tawhidi, ibada ya Mungu Mmoja.
6 - Al-Kafirun (The Disbelievers) - 006