Hakuna mtu yeyote atakayeshuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu nakuwa Muhammadi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa ukweli toka moyoni mwake, isipokuwa Mwenyezi Mungu atamharamishia moto
Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maalik -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Yakuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na Muadhi akiwa nyuma yake alisema: "Ewe Muadhi bin Jabali", Akasema: Labaika Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akasema hivyo mara tatu: " Hakuna mtu y…

