Siku moja mtu mmoja alikuwa akipita njiani akakuta tawi la miba likiwa njiani akaliondosha, Allah akamshukuru na akamfutia madhambi yake
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Siku moja mtu mmoja alikuwa akipita njiani akakuta tawi la miba likiwa njiani akaliondosha, Allah akamshukuru na akamfutia madhambi yake".

