Hivi kwani hajakuwekeeni Mwenyezi Mungu mambo mnayoweza kutoa sadaka: Hakika katika kila tasbihi (kauli ya sub-haanallaah) ni sadaka, na kila takbira (Allahu Akbaru) ni sadaka, na kila tahmidi (Alhamdulillah) ni sadaka, na kila tahalili (Laa ilaaha illallaahu) ni sadaka, na kuamrisha mema ni sadaka, na kukataza maovu ni sadaka, na katika kiungo cha siri cha mmoja wenu kuna sadaka
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Dharri -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Yakwamba watu miongoni mwa Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake walisema kumwambia Mtume rehema na amani ziwe juu yake. Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wamechukua malipo mengi wenye ut…

