Ikiwa mmoja wenu atachukua kamba yake, akaleta mzigo wa kuni juu ya mgongo wake, akauuza, na Mwenyezi Mungu akausitiri uso wake, basi hilo ni bora zaidi kwake kuliko kuwaomba watu wampe au wamnyime
Kutoka kwa Zubair bin Awwam -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Ikiwa mmoja wenu atachukua kamba yake, akaleta mzigo wa kuni juu ya mgongo wake, akauuza, na Mwenyezi Mungu akausitiri uso wake, basi hilo ni bora zaidi…

