Hakika shetani alishakata tamaa kuabudiwa na wenye kuswali katika kisiwa cha Arab, Lakini yuko katika kuwachochea baina yao
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Imepokelewa kutoka kwa Jabiri -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakika shetani alishakata tamaa kuabudiwa na wenye kuswali katika kisiwa cha Arab, Lakini yuko katika kuwachochea baina yao".
Explanation
Benefits
Shetani anakwenda mbio katika kuchochea ugomvi na chuki na vita na fitina baina ya waislamu.
Miongoni mwa faida za swala katika Uislamu nikuwa inalinda mapenzi kati ya waislamu, na ikayatia nguvu mahusiano ya kiudugu baina yao.
Swala ndiyo nembo kubwa ya dini baada ya shahada mbili, na ndio maana wameitwa waislamu wanaoswali.
Kisiwa Arab kina mambo maalumu yasiyokuwepo katika miji mingine.
Ikiwa kutasema kuwa, mbona kumetokea katika baadhi ya Kisiwa Arab ibada za masanamu, hali yakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anasema: "Hakika Shetani amekwishakata tamaa ya kuabudiwa na wenye kuswali...", hii ni taarifa ya yale yaliyotokea katika nafsi ya Shetani katika kukata tamaa baada ya kuona ufunguzi wa miji mbali mbali, na watu kuingia ndani ya dini ya Mwenyezi Mungu makundi kwa makundi, hadithi imeeleza dhana ya Shetani na kutokea kwake, kisha uhalisia ukawa kinyume na matarajio kwa hekima aliyoitaka Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

