Pindi atakapaowakusanya Mwenyezi Mungu wa mwanzo na wa mwisho siku ya Kiyama itanyanyuliwa bendera kwa kila haini, patasemwa: Hii ndio hiana ya fulani bin fulani
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa bin Omari radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake, amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake: "Pindi atakapaowakusanya Mwenyezi Mungu wa mwanzo na wa mwisho siku ya Kiyama itanyanyuliwa bendera kwa kila haini, patasemwa: Hii ndio hiana ya fulani bin fulani".
Explanation
Benefits
Hiana iliyosemwa katika hadithi inakusanya kila aliyekuamini juu ya damu, au heshima, au siri, au mali, kisha ukamfanyia hiana, na ukaenda kinyume na dhana yake katika kukuamini kwake.
Amesema Qurtubi: Hili ni tamko kutoka kwake linawahusu waarabu kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyafanya; kwani wao walikuwa wakinyanyua bendera nyeupe kwa ajili ya kutimiza ahadi, na kwa usaliti bendera nyeusi, ili wamlaumu haini na wamkemee, hadithi ikapelekea kutokea mfano wa hilo kwa haini; ili awe mashuhuri kwa sifa yake hiyo siku ya Kiyama, na watamsema kwa ubaya waliosimama katika uwanja huo.
Amesema bin Hajari: Na katika hadithi hii nikuwa watu siku ya Kiyama wataitwa kwa ubini wa baba zao; kwa kauli yake aliposema: "Huu ni usaliti wa fulani bin fulani".
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

