Wema ni tabia njema, na dhambi ni lile lililokukereketa katika nafsi yako na ukawa hukupendezwa watu walione
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Imepokelewa kutoka kwa Nawwaas bin Sam'aan Al-Answaariy -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Wema ni tabia njema, na dhambi ni lile lililokukereketa katika nafsi yako na ukawa hukupendezwa watu walione". Na kutoka kwa Wabiswa bin Ma'bad -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Nilimjia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-, Akasema: "Umekuja kuuliza kuhusu wema?" Nikasema: 'Ndiyo' Akasema: "Uchunguze moyo wako, Wema ni ule ambao nafsi itatulizana kwake, na moyo ukatulizana, na uovu ni ule unaokereketa ndani ya nafsi, na ukawa unatia shaka ndani ya kifua, hata kama watu watakupa majibu mazuri kiasi gani".
Explanation
Benefits
Haki na batili haviwezi kumchanganya muumini, bali anaijua haki kwa nuru aliyonayo ndani ya moyo wake, na anaichukia batili na kuikataa.
Miongoni mwa alama za dhambi ni moyo kukosa utulivu na kuwa na shaka, na kuchukia watu wasilione.
Amesema As-Sanadi: Hii ni katika mambo yenye kutatiza ambayo watu hawajui kutofautisha moja kati ya pande mbili; na kama si hivyo basi kilichoamrishwa na sheria pasina kuonekana dalili ndani yake ni kinyume na hilo katika wema, na yaliyokatazwa hivyo hivyo miongoni mwa madhambi, na hayo hakuna haja ya kuuliza ama kuutazama moyo na kuona utulivu wake.
Wanaosemeshwa katika hadithi hii ni wale wenye maumbile salama (ambao mioyo yao na akili zao hazijavurugwa na fikra potofu), na si wenye mioyo iliyofunikwa isiyojua jema wala kulikataa ovu isipokuwa yale iliyonyweshwa katika matamanio yake.
Amesema Attwayibi: Inasemekana: Imefasiriwa maana ya wema katika hadithi kwa maana nyingi, akaifasiri katika baadhi ya sehemu kuwa ni yale ambayo nafsi imetulizana kwayo na moyo ukatuliza pia, na akaifasiri katika sehemu nyingine kuwa ni imani, na katika sehemu nyingine, kwa yale yanayokuweka karibu na Mwenyezi Mungu, na hapa ameifasiri kwa kuwa na tabia njema, na akafasiri tabia njema kuwa: Ni kuvumilia maudhi na kupunguza hasira, na kukunjua uso, na kuwa na maneno mazuri, na yote hayo yanakaribiana katika maana.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

