Kila kilevi ni haramu.
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Abuu Buraida, kutoka kwa baba yake kutoka kwa Abuu Musa A-Ash'ari radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimtuma kwenda Yemen, akamuuliza kuhusu vinywaji fulani vinavyotengenezwa huko, akasema: Ni vipi hivyo?, akasema: "Ni Bit'u na Mizru" akaulizwa Abuu Buraida: Bit'u ni nini? Akasema: Ni mvinyo wa Asali, na Mizru: Ni mvinyo wa ngano, akasema: "Kila kilevi ni haramu" Ameitoa Bukhari. Na ameitoa Muslim na tamko lake ni: Alisema: Alinituma Mtume rehema na amani ziwe juu yake mimi pamoja na Muadh kwenda Yemen, nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Kuna vinywaji hutengenezwa huko katika nchi yetu vinaitwa: Mvinyo wa Mizru hutengenezwa kwa ngano, na kinywaji kingine huitwa: Bit'u hutengenezwa kwa Asali, akasema: "Kila chenye kulewesha ni haramu". Na katika riwaya nyingine ya Muslim: "Akasema: "Kila chenye kulewesha dhidi ya swala ni haramu". Na katika riwaya yake nyingine: "Na alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kapewa maneno machache yenye kukusanya maana nyingi mwisho wake, akasema: Ninakataza kila kilevi chenye kulewesha dhidi ya swala".
Explanation
Benefits
Hadithi hii ni kanuni katika kuharamisha aina zote za vilevi kama pombe na bangi na nyinginezo.
Umuhimu wa kuuliza yale anayoyahitajia Muislamu.
Ilikuwa mwanzo ilipoharamishwa pombe ni wakati swala inapoingia, pindi waliposwali baadhi ya watu waliohamia Madina na wakasoma wakachanganya ndani ya kisomo chao; ikateremka kauli yake: "Enyi mlio amini! Msiikaribia swala hali nyinyi mmelewa mpaka mjue mnachokisema" [An Nisaa: 43]. Na alikuwa muadhini wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akinadi: Msiikaribie swala hali yakuwa mmelewa. Kisha Mwenyezi Mungu akaiharamisha moja kwa moja kwa kauli yake: "Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli ni uchafu katika kazi ya Shetani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa (90) Hakika Shetani anataka kutia kati yenu uadui na chuki kupitia ulevi na kamari, na akuzuieni kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kusali. Basi je, mmeacha?" [Al-Maidah: 90,91].
Nikuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu aliiharamisha pombe kulingana na madhara na maovu makubwa yaliyomo.
Kinachozingatiwa katika uharamu ni uwepo wa sifa ya kilevi; mvinyo ukisifika kwa sifa ya kilevi basi ni haramu, na usipokuwa na kilevi basi ni halali.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

