Hakika Mwenyezi Mungu aliandika mema na maovu, kisha akalibainisha hilo
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa bin Abbas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika yale anayoyapokea kutoka kwa Mola wake Mlezi Aliyetukuka amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu aliandika mema na maovu, kisha akalibainisha hilo, basi yeyote atakayepania jema akawa hakulifanya; Mwenyezi Mungu huliandika kwake kuwa ni jema kamili, na akilipania na akalifanya; basi Mwenyezi Mungu huliandika kwake kuwa ni mema kumi mpaka ziada mia saba mpaka nyongeza nyingi zaidi, na akipania baya akawa hakulifanya; Mwenyezi Mungu huliandika kwake kuwa ni jema moja kamili, na akikusudia na akalifanya; basi Mwenyezi Mungu huliandika kuwa ni ovu moja".
Explanation
Atakayetaka na akakusudia na akaazimia kufanya jema basi litaandikwa kwake jema moja, hata kama hatolifanya, na ikiwa atalifanya basi hulipwa mara dufu kwa mara kumi mfano wake, mpaka ziada ya mia saba, mpaka ziada nyingi zaidi, na ziada huendana na yale yaliyoko moyoni kwanzia Ikhlaswi (kutakasa nia) na kuwanufaisha wengine, n.k.
Na atakayetaka na akakusudia na akaazimia kufanya uovu kisha akauacha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, huanidikiwa jema moja, na ikiwa atauacha kwa sababu ya kukosa muda wa kuufanya na akiwa hajafanya sababu za kuuendea, hatoandikiwa chochote, na akiuacha kwa kushindwa huandikwa nia yake pekee, na ikiwa ataufanya litaandikwa kwa ovu moja.
Benefits
Umuhimu wa nia katika amali zote na athari yake.
Fadhila za Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka- na upole wake na ihisani yake nikuwa mwenye kudhamiria jema na akawa hakulifanya Allah huliandika jema kamili.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

