Hakika zitatokea fitina, kisha tambueni kuwa fitina ya aliyekaa ndani inanafuu kuliko anayetembea, na anayetembea ndani yake inanafuu kuliko anayeikimbilia,
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Othman As Shaham, amesema:Niliondoka mimi pamoja na Farqad As Sabakhi kwenda kwa Muslim bin Abii Bakara naye akiwa katika mji wake, tukaingia kwake na tukasema: Hivi uliwahi kumsikia baba yako akisimulia hadithi yoyote kuhusu fitina? Akasema: Ndiyo, Nilimsikia Abuu Bakra radhi za Allah ziwe juu yake akihadithia, akasema: Alisema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika zitatokea fitina, kisha tambueni kuwa fitina ya aliyekaa ndani inanafuu kuliko anayetembea, na anayetembea ndani yake inanafuu kuliko anayeikimbilia, tambueni itakapoteremka au ikatokea basi atakayekuwa na ngamia basi na amfuate ngamia wake, na atakayekuwa na mbuzi basi na amfuate mbuzi wake, na atakayekuwa na ardhi basi na aende katika ardhi yake", anasema, akasema mtu mmoja: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu wasemaje ikiwa mtu hana ngamia wala mbuzi wala ardhi? Akasema: "Basi achukue panga lake na apige upande wa makali yake katika jiwe, kisha aokoke akiweza kuokoka, ewe Allah je nimefikisha? ewe Allah je nimefikisha? ewe Allah je nimefikisha?" Akasema: Akasema mtu mmoja: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu wasemaje endapo nitalazimishwa mpaka nikapelekwa katika moja kati ya safu mbili, au moja kati ya makundi mawili, mtu mmoja akanipiga kwa panga lake, au ukanilenga mshale ukaniua? Akasema: "Yeye ndiye atakayebeba dhambi zake na dhambi zako, na atakuwa miongoni mwa watu wa motoni".
Explanation
Benefits
Amesema Nawawi: Kauli yake rehema na amani ziwe juu yake: "Aliyekaa ndani yake ni bora kuliko aliyesimama", mpaka mwisho wake, maana yake ni kubainishwa hatari yake, na himizo la kuiepuka, na kuikimbia, na kwamba shari yake na fitina yake inakuwa kulingana na namna mtu alivyofungamana nayo.
Amesema Nawawi: Kumeondolewa dhambi kwa aliyelazimishwa atakayehudhuria huko, na ama kuuwa si halali hata kwa kulazimishwa, bali aliyelazimishwa anapata dhambi kwa lile aliloamrishwa kwa makubaliano ya wanachuoni wote.
Amesema bin Hajari: Na wamesema wengine: Likifanya dhulma kundi likatoka kwa kiongozi likakataa kutekeleza wajibu wake na likaanzisha vita basi ni wajibu kulipiga vita, na vile vile yakipigana makundi mawili ni wajibu kwa kila mwenye kuweza kumzuia mkosefu na kumtetea aliyepigwa, na hii ndio kauli ya jopo la wanachuoni, na wamefafanua wengine, wakasema: Kila mapigano yatakayotokea kati ya makundi mawili ya waislamu kiasi kwamba hakuna kiongozi wa umma, basi hapo mapigano hayo ni marufuku, na zinashuka hadithi zote zilizopo katika mlango huu na nyinginezo.
Amesema Nawawi: Na wametofautiana wanachuoni katika mapigano ya fitina, kundi miongoni mwao wakasema: Hakuna kupigana katika fitina ya waislamu, hata wakiingia ndani ya nyumba yake, na wakataka kumuuwa, hairuhusiwi kwake kujihami; kwa sababu kamtaka hilo kwa ufahamu potofu, na hii ni kauli ya Abii Bakra Swahaba radhi za Allah ziwe juu yake na wengineo, na amesema bin Omari na Imrani bin Huswaini radhi za Allah ziwe juu yao: Haingii hapa, lakini akikusudia kujihami, kauli zote hizi mbili zimeafikiana juu ya kuacha kuingia katika fitina zote za Uislamu. Na wamesema Maswahaba wengi na wanafunzi wao na wanachuoni wote wa Uislamu: Ni wajibu kumtetea mwenye haki katika fitina, na kusimama naye kwa kupigana na adui jeuri, kama alivyosema Mtukufu: "Basi lipigeni kundi linalodhulumu mpaka lirejee kwenye amri ya Mwenyezi Mungu..." mpaka mwisho wa aya, na kauli hii ndiyo sahihi, na hadithi hii inafasiriwa kwa yule ambaye hajabainikiwa na haki, au juu ya makundi mawili dhalimu, na hakuna lolote lililoelewa vibaya aya au hadithi miongoni mwao.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

