Watakuja watawala, mtayajua baadhi ya matendo yao kuwa yanakwenda sawa na sheria, na mengine mtayakemea (kwa kuwa yako nje ya sheria) atakayelijua hilo ataepukana na dhima, na atakayekemea atasalimika, lakini atakayeridhia na akawafuata
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Ummu Salama mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake: Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Watakuja watawala, mtayajua baadhi ya matendo yao kuwa yanakwenda sawa na sheria, na mengine mtayakemea (kwa kuwa yako nje ya sheria) atakayelijua hilo ataepukana na dhima, na atakayekemea atasalimika, lakini atakayeridhia na akawafuata" Wakasema: Kwa nini tusiwapige vita? Akasema: "Hapana, (Msifanye hivyo) madam ni waislamu na wanasimamisha swala".
Explanation
Kisha wakamuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Kwa nini tusiwapige vita viongozi ambao wanasifa kama hizi? Akawakataza wasifanye hivyo, na akasema: Hapana, msifanye hivyo madama wanasimamisha swala kwenu nyinyi.
Benefits
Haifai kuridhia uovu wala kushiriki ndani yake, na ni lazima kuukemea.
Watakapozua viongozi mambo yanayokwenda kinyume na sheria haitakiwi kuwatii katika hilo.
Kutofaa kujitoa chini ya viongozi wa waislamu; kwakuwa hilo linaambatana na madhara na umwagaji damu na amani kutoweka, kuvumilia uovu wa viongozi watenda maasi, na kusubiri juu ya kero zao, haya ni mepesi kuliko kuvunja amani na kumwaga damu.
Swala ina nafasi kubwa, ndio inayotenganisha kati ya ukafiri na Uislamu.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

