HadeethEnc · 1.18.0
Asiashirie mmoja wenu silaha kwa ndugu yake, kwani hajui, huenda Shetani akaipokonya kutoka mkononi mwake, akatumbukia katika shimo la moto
Available translations
Choose an available translation of this Hadeeth
01
Hadeeth text
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Asiashirie mmoja wenu silaha kwa ndugu yake, kwani hajui, huenda Shetani akaipokonya kutoka mkononi mwake, akatumbukia katika shimo la moto".
02
Explanation
Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake muislamu kuashiria juu ya ndugu yake muislamu kwa silaha, kwa aina yoyote ile miongoni mwa aina za silaha, kwa sababu yeye hajui huenda Shetani akamsukuma kuitikisa silaha mkononi mwake, akamuuwa ndugu yake au akamuudhi, akatumbukia katika maasi yanayoweza kumpelekea kuingia katika shimo la moto.
03
Benefits
Kumebainishwa uharamu wa damu muislamu.
Ulazima wa kumheshimu muislamu na tahadhari ya kumfikishia shari kwake kwa kitendo au kauli, ikiwemo kumuashiria kwa chuma au silaha, hata kama ni kwa mzaha; kwa sababu Shetani anaweza kuutelezesha mkono wake na akampendezeshea kumpiga ndugu yake, au akaipokonya silaha kutoka mkononi mwake ikatua pasina maamuzi yake ikamdhuru ndugu yake.
Kuziba njia zinazopelekea katika jambo kwa kukataza yanayopelekea katika haramu.
Pupa ya kuhakikisha usalama wa jamii na kuhifadhi mahusiano baina ya watu, na kutowatisha na kuwaogopesha hata kama ni kwa ishara na kutishia.

Attribution
[Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake]
Categories
Share
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares