Achaneni (na ubaguzi) kwani una nuka
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Jaabir bin Abdillaah -radhi za Allah ziwe juu yao (yeye na baba yake), amesema: Tulikuwa vitani, mtu mmoja katika Muhajirina akampiga mmoja katika Answari, Answari akasema: Maanswari naombeni msaada!, na akasema Mhajiri (mtu wa Makka): Naombeni msaada enyi Muhajirina!, Mwenyezi Mungu akamsikilizisha sauti zile Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake, akasema: "Nini hiki?" Wakasema: Mtu mmoja miongoni mwa Muhajirina kampiga mtu katika Maanswari, akasema Answari: Naombeni msaada enyi Maanswari, na akasema Mhajiri: Naombeni msaada enyi Muhajirina, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Achaneni (na ubaguzi) kwani una nuka" Amesema Jabiri: Na Maanswari walikuwa wengi kipindi alipofika Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kisha Muhajirina wakawa wengi baada ya hapo, akasema Abdallah bin Ubaiyi: Vipi wamepigana? Na Wallahi tukirejea Madina watukufu watawafurusha madhalili, akasema Omari bin Khattwabi: Naomba uniache mimi ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu nikate shingo ya huyu mnafiki, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Muache ili watu wasiseme Muhammadi anauwa Maswahaba zake".
Explanation
Benefits
Kuchukua tahadhari dhidi ya kuwa na kundi la batili, na kuliepuka ni sawa na kukiepuka kitu kibaya kinachonuka.
Katazo la kila chenye kuamsha uadui na chuki.
Amesema Nawawi: Mtume rehema na amani ziwe juu yake kukiita kwake kitendo kile kuwa ni madai ya kijinga ni kwa sababu ya kukichukia, kwa sababu ni vitendo walivyokuwa navyo zama za ujinga, kama kupeana nguvu kwa makabila katika mambo ya kidunia na yahusianayo na dunia, na zama za ujinga walikuwa wakichukua haki zao kwa ukoo na makabila, Uislamu ukaja kuyabatilisha haya, na kusuluhisha kesi zote kwa hukumu za kisheria, hivyo, mtu akimtendea ubaya mwenzake hakimu atawahukumu, na atamlazimisha lolote kulingana na uadui wake alioufanya, kama ilivyothibitshwa katika kanuni za Uislamu.
Amesema Sandi: Akabainisha kuwa usaidizi madamu ni kutoka katika kabila lake basi ni batili, hakuna haja ya kuita kila mmoja kabila lake, na ama kuitetea haki ni jambo linahitajika bali ni lazima kwa kila muumini sawa sawa awe ni kabila lake au la.
Hali waliyokuwa nayo wanafiki kama kuwa na ulimi mchafu na ujasiri kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kwa Maswahaba zake radhi za Allah ziwe juu yake.
Upole mkubwa wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na subira yake kwa maudhi ya wanafiki anayoyapata.
Tahadhari ya kila jambo ambalo ndani yake linawakimbiza watu katika Uislamu, na ndio mana alikataa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwaua wanafiki, ili watu wasiseme: Kuwa Muhammadi anauwa Maswahaba zake.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

