Hakuna yeyote katika Manabii isipokuwa alipewa mfano wa yale waliyoyaamini watu
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake: "Hakuna yeyote katika Manabii isipokuwa alipewa mfano wa yale waliyoyaamini watu, na hakika niliyopewa mimi ni wahyi (ufunuo) wa Mwenyezi Mungu alionifunulia, basi nataraji kuwa na wafuasi wengi kuliko wao siku ya Kiyama".
Explanation
Benefits
Kumebainishwa ukubwa wa muujiza wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
Kumebainishwa ukubwa wa nafasi ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake na ubora wake juu ya Manabii wengine.
Amesema bin Hajari katika kauli yake: "Bali imekuwa kile nilichopewa kuwa ni wahyi alioniteremshia Mwenyezi Mungu kwangu mimi": Na makusudio yake si kubana miujiza yake hapa, wala kuwa hakupewa miujiza waliopewa waliomtangulia, bali makusudio yake ni kuwa ndio muujiza mkubwa ambao ulikuwa maalumu kwake peke yake pasina mwingine.
Amesema Nawawi: "(Nataraji mimi kuwa na wafuasi wengi zaidi yao" Hii ni alama miongoni mwa alama za Unabii, kwani alilieleza hili rehema na amani ziwe juu yake katika zama za Waislamu wachache, kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akaleta neema na akawafungulia Waislamu na akawabariki mpaka Uislamu ukafika mbali na ukapanuka kwa Waislamu kwa kiwango hiki kinachofahamika, tunamshukuru Mwenyezi Mungu.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

