Namuapa yule ambaye nafsi ya Muhammadi iko mkononi mwake, hatonisikia yeyote katika umma huu, Myahudi wala Mkristo, kisha akafa haliyakuwa hajayaamini yale niliyotumwa kwayo, isipokuwa atakuwa ni katika watu wa motoni
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -sala na amani ziwe juu yake- amesema: "Namuapa yule ambaye nafsi ya Muhammadi iko mkononi mwake, hatonisikia yeyote katika umma huu, Myahudi wala Mkristo, kisha akafa haliyakuwa hajayaamini yale niliyotumwa kwayo, isipokuwa atakuwa ni katika watu wa motoni".
Explanation
Benefits
Atakayempinga Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- hayatomfaa kitu madai yake ya kudai kumwamini Nabii mwingine katika Manabii -Amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yao wote-.
Ambaye hakumsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na haukumfikia ujumbe wa Uislamu huyu atapewa udhuru, na hukumu yake huko Akhera itakuwa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Yanathibitika manufaa kwa Uislamu kwa mtu hata kama atasilimu muda mchache kabla ya kifo, hata kama atakuwa katika maradhi mabaya, madama tu roho haijafika kooni.
Kuiona kuwa ni sahihi dini ya makafiri -wakiwemo Mayahudi na Wakristo- ni ukafiri.
Amemtaja Myahudi na Mkristo katika hadithi kama tahadhari kwa wenye kuwaona kuwa wako sawa; na hii ni kwakuwa Mayahudi na Wakristo wana kitabu, na ikiwa ndio hivyo, basi kwa wengine wasiokuwa na kitabu ndio wanastahiki zaidi kuingia motoni, wote hao wanalazimika kuingia katika dini yake na kumtii yeye Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

