Amekwisha ionja ladha ya imani, yule mwenye kumridhia Mwenyezi Mungu kuwa ndiye Mola wake, na Uislamu ndiyo dini, na Muhammad ni Mtume
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Abbasi bin Abdil Muttwalib radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba yeye alimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Amekwisha ionja ladha ya imani, yule mwenye kumridhia Mwenyezi Mungu kuwa ndiye Mola wake, na Uislamu ndiyo dini, na Muhammad ni Mtume"
Explanation
La kwanza: Akiridhika kuwa Mwenyezi Mungu ni Mola wake Mlezi, na hii ni kwa kukunjuka kifua chake kwa yale yanayomfikia kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa muktadha wa ulezi, ikiwemo kugawa riziki na hali za waja, asipate upinzani kwa kitu chochote ndani ya nafsi yake, na asitafute Mola Mlezi zaidi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
La pili: Aridhie kuwa Uislamu ndio Dini ya kweli, na hii ni kwa kukunjuka kifua chake kwa yale yanayofungamana na Uislamu kama sheria na wajibu, na asipite njia nyingine isiyokuwa Uislamu.
La tatu: Aridhie kuwa Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake ni Mtume, na hii ni kwa kukunjuka kifua chake na afurahie yote aliyokuja nayo pasina kusitasita wala kutia shaka, na asipite ila njia inayokwenda sambamba na muongozo wake rehema na amani ziwe juu yake.
Benefits
Mwili haupati ladha ya chakula na kinywaji isipokuwa unapokuwa na afya njema, hivyo hivyo hata moyo ukisalimika na maradhi ya matamanio potofu, na matamanio yaliyoharamishwa, utapata utamu wa imani, na utakapougua na nakuwa mgonjwa kamwe hauwezi kupata utamu wa imani, bali unaweza kupata utamu wa mambo yanayoangamiza kama matamanio na maasi.
Mwanadam atakaporidhia jambo na akaliona kuwa zuri linakuwa jepesi kulifanyia kazi, na wala hakuna kitakachoweza kumpa tabu katika hilo, na atafurahia kwa kila kilichokuja katika jambo hilo, na bashasha itaingia ndani ya moyo wake, hivyo hivyo hata muumini imani inapoingia ndani ya moyo wake, huwa rahisi kwake kumtii Mola wake Mlezi na nafsi yake huhisi ladha, na hakuna tabu zitakazomuwia ugumu.
Amesema Ibnil Qayyim: Hadithi hii imekusanya kuridhia uumbaji na upangiliaji wake Mtukufu na uungu wake, na kuridhika na Mtume wake na kumtii, na kuridhika na dini yake na kujisalimisha kwa dini hiyo.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

