Andika, namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakitoki ndani yake ila haki
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Abdallah bin Amri -Radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake- amesema: Nilikuwa nikiandika kila kitu ninachokisikia kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- nikitaka kukihifadhi, Makuraishi wakanikataza, na wakasema: Hivi unaandika kila kitu unachokisikia kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni mwanadamu huzungumza wakati wa hasira na furaha? Nikaacha kuandika, nikamueleza hilo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akaashiria kwa kidole chake katika kinywa chake, akasema: "Andika, namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakitoki ndani yake ila haki".
Explanation
Nikamueleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- waliyosema, akaashiria kwa kidole chake kinywani kwake akasema: Andika, namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake haitoki ndani yake ila haki kwa hali zote, na katika furaha na hasira.
Na alisema Mtukufu kumuhusu Nabii wake -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Na hatamki kwa matamanio * Si vinginevyo, ila huo ni wahyi anaofunuliwa" [An najm: 3-4].
Benefits
Pupa ya Masahaba radhi za Allah ziwe juu yao katika kuihifadhi sunna na kuifikisha.
Kufaa kuapa hata kama hakuna masilahi katika hilo, kama kulitilia mkazo jambo.
Kuiandika elimu ni katika sababu kubwa zinazoihifadhi elimu.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

