Akasema: "Watahesabiwa kwa hiyana waliyokufanyia na kukuasi na kukudanganya, na itahesabiwa adhabu yako uliyowapa
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Imepokelewa kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Ya kuwa mtu mmoja alikaa mbele ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwa hakika mimi nina watu niliowamiliki, wakati mwingine wananidanganya na wananifanyia hiyana na wanakwenda kinyume na amri zangu, nahuwa nawatia adabu kwa kuwatukana na kuwapiga, hivyo naulizia kuwa ni vipi itakuwa hali yangu kwa kuwafanyia hayo?Akasema: "Watahesabiwa kwa hiyana waliyokufanyia na kukuasi na kukudanganya, na itahesabiwa adhabu yako uliyowapa basi ikiwa adhabu uliyowapa ipo sawa na makosa yao basi itatosha na hapatakuwa na chochote kwako wala kwao, na ikiwa adhabu uliyowapa ni ya chini kulingana na kosa walilofanya basi utalipwa na utazidishiwa kwenye malipo yako, na ikiwa umewaadhibu zaidi ya walivyokosea yatapunguzwa kutoka kwako malipo ya ziada" Akasema: Basi yule bwana alijitenga na akawa analia kwa sauti ya juu, Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akamwambia: "Hivi husomi katika kitabu cha Mwenyezi Mungu aliposema: "Na Sisi tutaweka Mizani ya uadilifu siku ya Kiyama na hakuna nafsi yoyote itakayodhulumiwa kwa chochote", mpaka mwisho wa Aya, yule bwana akasema: Nakuapia ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, sijaona kheri iliyopo kati yangu na yao zaidi ya kuwaachia huru, na ninakupa ushuhuda kuwa wao wote kuanzia sasa wako huru".
Explanation
Benefits
Inafaa kumuadhibu dhalimu ikiwa adhabu hiyo itakuwa sawa na makosa yake au kumwadhibu adhabu ndogo ikilinganishwa na kosa lake, ama kumzidishia adhabu ni haramu na haifai.
Himizo la kuamiliana vizuri na watumishi na watu madhaifu.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

