Hakika Mwenyezi Mungu anapompenda mja humuita Jibril na husema: Hakika mimi ninampenda fulani basi mpende, anasema: Jibril humpenda
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu anapompenda mja humuita Jibril na husema: Hakika mimi ninampenda fulani basi mpende, anasema: Jibril humpenda, kisha anaita huko mbinguni na kusema: Hakika Mwenyezi Mungu anampenda fulani basi mpendeni, wanampenda wakazi wa mbinguni, anasema kisha anapewa kukubalika katika Ardhi, na anapomchukia mja humuita Jibril na kusema: Hakika mimi ninamchukia fulani basi mchukie, anasema; Basi Jibril humchukia, kisha ananadi kwa wakazi wa mbinguni; hakika Mwenyezi Mungu anamchukia fulani basi mchukieni, anasema: basi wanamchukia, kisha anawekewa kuchukiwa katika Ardhi".
Explanation
Benefits
Atakayependwa na Mwenyezi Mungu basi watampenda wakazi wa mbinguni na ardhini, na atakayemchukia Mwenyezi Mungu watamchukia wakazi wa mbinguni na ardhini.
Amesema Assanadi: Kauli yake: "Na atawekewa kukubalika katika Ardhi", si lazima wamkubali watu wote, bali ni kwa kiwango alichokitaka Mwenyezi Mungu kwake cha kukubalika katika Ardhi, ndivyo hivyo kwa sababu uadui wa watu waovu kwa watu wema unafahamika.
Himizo la kutimiza amali za wema kwa namna zake tofauti tofauti, za faradhi za sunna, na tahadhari ya maasi na uzushi; kwa sababu ndio huchukuliwa kama sababu ya kupata hasira.
Amesema bin Hajari: Na inachukuliwa hapa kuwa mapenzi ya nyoyo za watu ni alama ya mapenzi ya Mwenyezi Mungu, na inaungwa mkono na hadithi ya jeneza, aliyosema Mtume: "Nyinyi ndio mashahidi wa Mwenyezi Mungu katika Ardhi".
Amesema binil Arabi Al-Maaliki: Na inakusudiwa wakazi wa ardhi wale wanaomfahamu pasina wasiomfahamu wala kuwahi kumsikia.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

