Mambo mawili kwa watu hayo kwao ni ukafiri: Kutiana doa katika nasaba (ukoo), na kulia kwa kumuomboleza maiti
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Mambo mawili kwa watu hayo kwao ni ukafiri: Kutiana doa katika nasaba (ukoo), na kulia kwa kumuomboleza maiti".
Explanation
La kwanza: Kutukana nasaba (koo) za watu na kuzishushia heshima na kujikweza juu yao.
La pili: Kunyanyua sauti wakati wa msiba kwa kulalamika juu ya kadari, au kukata nguo kwa sababu ya mfadhaiko mkubwa.
Benefits
Ulazima wa kusubiri juu ya msiba na kutolalamika.
Matendo haya ni katika ukafiri mdogo, na si kwamba mwenye kufanya sehemu katika sehemu za ukafiri anakuwa kafiri ukafiri unaomtoa mtu katika mila ya Uislamu mpaka umthibitikie ukafiri mkubwa.
Uislamu umekataza mambo yote yanayopelekea kutengana baina ya waislamu kama kutukana nasaba na mengineyo.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

