Enyi watu, toleaneni salamu na muunge udugu, na mlishe chakula, na msali usiku watu wakiwa wamelala, mtaingia peponi kwa amani
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Abdullah bin Salam radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alipokuja Madina Mtume rehema na amani ziwe juu yake, watu walikusanyika mbele yake, pakasemwa: Amefika Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake, Amefika Mtume wa Mwenyezi Mungu, Amefika Mtume wa Mwenyezi Mungu, wakasema mara tatu, nikaja pamoja na watu kutazama, na nilipouona uso wake nikajua kuwa uso wake si uso wa muongo, kwa hivyo jambo la kwanza nililomsikia akizungumza alisema kuwa: "Enyi watu, toleaneni salamu na muunge udugu, na mlishe chakula, na msali usiku watu wakiwa wamelala, mtaingia peponi kwa amani".
Explanation
La kwanza: kusambaza salamu ya amani, na kuionyesha na kuikithirisha kwa wale unaowajua na usiowajua.
La pili: Kulishiza chakula kwa sadaka na zawadi na kukaribisha ugeni.
La tatu: Kuunga udugu kwa wale kinachowaunganisha kizazi au ukaribu wa udugu upande wa baba au mama.
La nne: Swala za sunna, kisimamo cha usiku na watu wakiwa wamelala.
Benefits
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

