Hakika Mwenyezi Mungu amemuwajibishia pepo kwa kile alichokifanya, au amemuacha huru na moto kwa kile alicho kifanya
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Alinijia mwanamke mmoja Masikini akiwa amebeba mabinti zake wawili, nikawalisha tende tatu, akawapa kila mmoja wao tende moja, kisha akanyanyua tende moja ili kuitumia , akawalishi mabinti zake kwa kuigawa tende ile vipande viwili, ambayo alihitaji kuila mwenyewe, kikanistaajabisha kitendo chake hicho, nikamueleza Mtume alicho kifanya mwanamke yule, akasema: "Hakika Mwenyezi Mungu amemuwajibishia pepo kwa kile alichokifanya, au amemuacha huru na moto kwa kile alicho kifanya".
Explanation
Benefits
Ukubwa wa huruma ya akina mama kwa watoto, na hofu yao juu ya kuwapoteza.
Fadhila za kuidhiki nafsi kwa kuwapendelea wengine, na kuwahurumia wadogo, na ziada ya wema na upole kwa watoto wa kike, na kwamba hilo ni sababu ya kuingia Peponi, na kuachwa huru na Moto.
Kitu kidogo hakizuiliwi kutolewa sadaka kwa sababu ya kubezwa kwake, bali ni wajibu kwa amtoaji sadaka atoe sadaka kwa kiasi anachokiweza kiwe kidogo au kikubwa.
Hapa kumeelezwa hali zilivyokuwa nyumba za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na vipi yalikuwa maisha yake na familia yake, kiasi kwamba hapakuwa na chochote cha kuliwa ndani ya nyumba zao, zaidi ya tende moja au tatu.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

