Kutoka kwa Abdillah bin Mas'udi -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Shikamaneni na ukweli, kwani ukweli hupelekea katika wema, na hakika wema hupelekea katika pepo
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: Kutoka kwa Abdillah bin Mas'udi -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Shikamaneni na ukweli, kwani ukweli hupelekea katika wema, na hakika wema hupelekea katika pepo, na hatoacha mtu kuwa mkweli na akishughulika na ukweli mpaka ataandikwa kwa Mwenyezi Mungu kuwa ni mkweli, na tahadharini na uongo, kwani uongo unapelekea katika uovu, na hakika uovu hupelekea katika moto, na hatoacha mtu kuendelea kuwa muongo, na akishughulika na uongo mpaka ataandikwa mbele ya Mwenyezi Mungu kuwa ni muongo".
Explanation
Benefits
Uongo ni tabia ya kulaumiwa ambayo mhusika huipata kupitia mazoea ya muda mrefu katika maneno na matendo, mpaka inakuwa ni tabia na silika yake, kisha anaandikwa mbele ya Mwenyezi Mungu kuwa ni katika waongo.
Ukweli unahusu ukweli wa ulimi, ambao ni kinyume cha uongo, na ukweli katika nia, ambao ni ikhlasi, na ukweli katika kusuluhisha vyema nia yake, na ukweli katika vitendo, na kwa uchache zaidi ni siri yake na dhahiri yake viwe sawa, na ukweli katika matukio kama kusema ukweli wakati wa hofu na raha, na mengineyo, hivyo yeyote atakayesifika na sifa hizo basi atakuwa ni mkweli mno, au akasifika na baadhi yake atakuwa mkweli pia.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

